TTCL

EQUITY

Monday, October 26, 2015

TUME YA TAIFA KUHESABU KURA ZA URAIS TANZANIA

Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam
 
15.38pm:Waandishi wa habari wajiandaa tayari kwa matokeo ya uchaguzi mkuu katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
 

17.16pm:Muungano wa upinzani nchini Tanzania UKAWA umedai kwamba vijana wake 200 ambao walikuwa wakikagua matokeo yanayotolewa kutoka kwa maajenti wake katika vituo vya kupiga kura kote nchini walikamatwa usiku uliopita na sasa wako kizuizini.

Naibu mwenyekiti wa muungano huo Profesa Abdalla Safari amesema kuwa vijana hao walikamatwa wakati maafisa wa polisi walipovamia vituo vya uchaguzi vya upinzani na kuchukua data muhimu na kompyuta.

Muungano huo umedai kwamba hatua hiyo ya maafisa wa polisi itawalazimu kupinga matokeo yoyote yatakayotolewa na tume ya uchaguzi NEC, ukisema kuwa umewachwa bila ushahidi wa kuonyesha kwamba kuna udanganyifu katika matokeo ya uchaguzi.

Umesema kuwa hautakubali matokeo hayo huku profesa Simba akisema kuwa uwezo wa raia utaamua mwelekeo wa taifa iwapo matokeo hayo hayatawapendelea.
Maelekezo kwa lugha mbili.kichina na kiingereza katika jumba la mikutano la Julius Neyerere jijini Dar es Salaam

14.25pm:Maelekezo katika jumba la mikutano la Julius Nyerere mjini Dar es Salaam yameandikwa kwa lugha mbili,kichina na kizungu.toa maoni yako

Njia iliofungwa kisiwani Zanzibar
13.29pm:Baadhi ya barabara katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa na maafisa wa polisi ili kukabiliana na matukio yoyote ya ghasia kisiwa ni humo.



Ukumbi wa matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar
13.19pm:Raia wamekongamana katika ukumbi wa matokeo kisiwani Zanzibar wakisubiri kutangazwa kwa washindi na tume ya uchaguzi kisiwani humo ZEC.



13.16pm:Upigaji kura unaendelea katika vituo vyengine 42 kati ya zaidi ya vituo 60,000 baada ya kushindwa kupiga kura siku ya jumapili kutokana na matatizo tofauti.

Maafisa wa polisi
13.12pm:Maafisa wa polisi wamepiga kambi nje na maeneo ya ukumbi wa mikutano wa Julius Neyerere ambapo matokeo ya kura yameanza kutangazwa.

Moody Awori kiongozi wa ujumbe wa waangalizi Afrika mashariki
12.54pm:Moody Awori ambaye ndio kiongozi wa ujumbe wa waangalizi kutoka Afrika Mashariki amewasili katika kituo cha kutangaza matokeo ya kura kilichopo katika jengo la Julius Nyerere jijini Daresalaam.

10.56am:Kuna hali ya wasiwasi mjini Mwanza huku maafisa wa polisi wakikabiliana na vijana wanaodaiwa kutoka katika chama cha UKAWA. Kuna visa ambapo vikosi vya usalama vilirusha gesi za kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.

Mwanza
10.24am: Hali ya kawaida imeanza kurudi mjini Mwanza huku biashara zikifunguliwa. Maduka yalikuwa mahame huku kile kilichojulikana kama mji uliokuwa na harakati nyingi ukibadilika na kuwa mahame.

Julius Nyerere
10.19am:Tume ya uchaguzi imeanza kutangaza  matokeo ya urais mapema leo, tangu saa tatu asubuhi katika jumba la mikutano la Julius Nyerere mjini Dar es Salaam

Maafisa wa usalama huko Mwanza
10.15am: Ulinzi mkali umewekwa kote nchini Tanzania huku tume ya uchaguzi ya taifa hilo ikianza kutoa matokeo ya uchaguzi.

Vijana wailalamikia tume ya uchaguzi
9.35am:Hawa ni baadhi ya vijana walioajiriwa na tume ya uchaguzi kufanya kazi kadhaa wakati wa uchaguzi katika eneo la Mwanza .Wameishtumu tume ya uchaguzi kwa kuwanyima marupurupu yao.




9.28am: Wazee na walemavu ndio watu walioathirika zaidi na tataizo hilo kwa kuwa iliwabidi wangojee tena.Hatahivyo wamewasili katika kituo hicho.

8.45am: Hatimaye wakaazi wa eneo la Kimara Stop Over mjini Dar es Salaam wameanza kupiga kura baada ya shughuli hiyo kukwama siku ya jumapili wakati maafisa wanaosimamia shughuli hiyo kutofautiana na wale wa tume ya uchaguzi na hivyobasi kuchoma vifaa vya kupigia kura.

7:20am: Usalama umeimarishwa katika kituo kikuu cha kujumlisha matokeo katika ukumbi wa Julius Nyerere. Tume inatarajiwa kutoa matokeo ya kwanza saa tatu.
Masanduku ya kupigia kura
7:15 am: Mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania, masanduku ya kura yanaendelea kukusanywa katika afisi kuu kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuhesabu kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imesema itaendelea kutoa matokeo  ya uchaguzi wa urais leo kutokana na yanavyo wafikia. Hata hivyo kuna maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika Jumapili hivyo yamefanyika leo hii, na bado zoezi la kuhesabu linaendelea na baadae kupeleka majumuisho katika majimbo yao ilikutumwa katika tume ya uchaguzi Dar es salaam.
 Bonyeza hapa kwa habari za karibu zaidi kuhusu matokeo ya kura

No comments:

Post a Comment