Wananchi katika
kituo cha kupigia kura cha Kimara Stop Over A na B mjini Dar es Salaam
wanaendelea kupiga kura baada ya kuahirishwa kwa shughuli hiyo hapo jana
kutokana na upungufu wa vifaa.
Hatua hiyo inajiri baada ya
maafisa walioteuliwa na tume ya uchaguzi kusimamia kituo hicho
kutofautiana kuhusu nyongeza ya marupurupu yao na hivyobasi kuchoma
makaratasi ya kupigia kura pamoja na sajili zake.
Lakini kufikia mapema leo maafisa wa tume ya uchaguzi walipeleka vifaa vyengine vya shughuli hiyo na kukubaliana na maafisa hao.
Awali wakaazi walikasirishwa na kucheleweshwa kwa shughuli hiyo wakilazimika kusubiri kabla ya zoezi hilo kuanza.
No comments:
Post a Comment