Waziri wa Viwanda
na Biashara Dkt Abdallah Kigoda alifariki dunia siku ya Jumatatu nchini
India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Bunge la
Tanzania Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa
Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi
nchini India Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge,
kimesema taarifa zaidi kuhusu msiba na taratibu za kurejesha mwili
nchini Tanzania zitaendelea kutolewa na Serikali na Ofisi ya Bunge kwa
kushirikiana na familia ya marehemu kadiri zinavyoendelea kupatikana
No comments:
Post a Comment