TTCL

EQUITY

Tuesday, October 13, 2015

Mwanamume aliyenunua Google $12 azawadiwa

Google

Mwanamume mmoja aliyefanikiwa kununua na kumiliki anwani ya Google.com kwenye mtandao kwa $12 pekee mwezi uliopita amezawadiwa na kampuni hiyo.
Mwanamume huyo Sanmay Ved aligundua udhaifu kwenye mfumo wa kiutawala wa Google na akanunua anwani hiyo Septemba 29.
Hilo lilimpa udhibiti wa anwani hiyo kwa dakika moja hivi kabla ya Google kugundua na kumpokonya.
Sasa, Bw Ved, ambaye ni mwanafunzi chuo nchini Marekani amezawadiwa pesa na kampuni hiyo kwa kugundua kosa hilo.
Ameamua kutoa pesa hizo, ambazo kiasi chake hakikufichuliwa, kwa mashirika ya kusaidia wasiojiweza katika jamii.
Google wamekataa kuzungumzia kisa hicho.
Bw Ved alisimulia matukio hayo kwenye ujumbe mtandao wa LinkedIn na kusema amekuwa akifuatilia anwani za Google kwa makini sana kwa muda mrefu. Aliwahi kufanya kazi wakati mmoja na shirika hilo
Mapema Septemba 29, aligundua kulikuwa na ujumbe wa ‘inauzwa’ karibu na anwani ya Google.com akichakura tovuti ya kununua anwani za mitandao kwenye tovuti ya uhunuzi wa mitandao hiyo inayomilikiwa na Google.
Alitumia kadi ya benki kulipa $12 (£8) fna akajitwalia anwani hiyo ya google.com.
Alipokea hata barua pepe ya kuthibitisha kwamba alikuwa amechukua umiliki.
Mara moja, alianza kupokea barua pepe zinazofaa kupokewa na wasiwamizi wa Google.
Lakini muda mfupi baadaye, alipokea barua ya kumfahamisha kwamba ununuzi wake ulikuwa umebatilishwa.
Alirejeshewa pesa zake.
Lakini baadaye alizawadiwa pesa kwa kusaidia Google kugundua udhaifu kwenye mifumo yake.
Bw Ved aliamua kutoa pesa zake kwa wakfu wa elimu India, hatua iliyofanya Google kuongeza zawadi yake maradufu.

No comments:

Post a Comment