Mwanamke mmoja raia
wa China aliyekamatwa kwa makosa ya ulanguzi wa pembe za ndovu zenye
thamani ya dola milioni mbili u nusu amenyimwa dhamana na mahakama moja
hapa Dar es Salaam.
Upande wa mashtaka umedai kuwa bi Yang Feng
Glan ndiye aliyekuwa akisimamia njama yote ya usafirishaji wa pembe za
ndovu kinyume cha sheria mbali na makosa mengine ya uhalifu.
Kimsingi
bi Feng Glan ndiye aliyekuwa bosi katika genge la majambazi
walioshiriki uwindaji haramu na matukio mengine ya wizi wa kupangwa wa
kimabavu.
Wachunguzi wameishawishi mahakama kuwa japo bi Yang Feng
Glan anasifika kwa kuendesha kwa ufanisi biashara ya mikahawa na
ukulima lakini pia ni mvunjaji mkubwa wa sheria.
Utawala hapa
Tanzania umempa bibi huyu hadhi ya 'Malkia wa pembe za ndovu'' baada ya
kuchunguza na kufwatilia nyendo zake kwa zaidi ya mwaka mmoja katika
uchunguzi uliokamilika alipokamatwa jijini
Dar es Salaam juma lililopita.
Vyombo
vya dola hapa vinadai kuwa Feng Glan ndiye mfadhili mkuu wa uwindaji
haramu wa ndovu mbali na ulanguzi wa wa zaidi ya pembe 700 za ndovu
katika kipindi cha miaka 14.
Mashirika yanayopigania uhifadhi wa
mazingira na wanyama pori nchini Tanzania wamefurahishwa na hatua ya
serikali kumchukulia hatua mchina huyo.
Mashirika hayo hata hivyo yanasema sharti Feng Glan
aukabili mkono wa sheria ili iwe mfano kwa wahusika wengine wa biashara
hiyo mbaya ya uwindaji haramu kwa ustawi wa wanyama pori.
Mwaka
uliopita shirika moja la uhifadhi wa mazingira na wanyama pori lenye
makao yake nchini Uingereza (Environmental Investigation Agency)
lilichapisha ripoti ya utafiti iliyoonyesha kuwa Tanzania ilipoteza
thuluthi mbili ya ndovu wake katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
katika kipindi hichi uchunguzi ulidai mahakamani kuwa bibi Feng alikuwa akiendesha genge la wawindaji haramu.
Iwapo atapatikana na hatia bi Feng anakabiliwa na hukumu ya miaka 30
No comments:
Post a Comment