Akiwa Diwani mteule wa kata ya Themi Jimbo la Arusha Mjini
2013 Ndugu Melance Kinabo (KABURU) kupitia CHADEMA, Kwa uchungu mkubwa alianza
kazi zake rasmi kama diwani hili hali bado hakuwa ameapishwa.Leo tarehe 29 -
June 2013 mishale ya saa tisa alasiri na kuwasili mtaa wa Fire maeneo ya
magorofa ya polisi kusikiliza kilio cha akina mama ambao ni wakulima wa
mbogamboga waliomuita kwa simu kumuomba msaada baada ya mwenyekiti wa Mtaa wa
Themi Magharibi Mzee Dions Msele - CCM kukataza matumizi ya mfereji wa kumwagia
maji ktk mashamba ya kina mama wa mtaa husika bila sababu za msingi.
Diwani huyu wa Themi kupitia Chadema aliwahoji akina mama husika na kugundua kuwa Mwenyikiti wa mtaa hakuwa na sababu za msingi za kuwazuiya kina mama hao kuendelea na kilimo cha umwagiliaji kupitia mfereji husika.
Diwani huyu mteulealipofika kwa mtendaji wa kata ya Themi aligundua kuwa kina mama hawa wa Themi Magharibi wananyanyaswa na mwenyekiti wa mtaa Dions Msele - CCM na ndipo akatoa amri kuwa mfereji huo ufunguliwe na kina mama waendelee na kilimo cha mboga bila kusumbuliwa na kutoa ahadi ya kusimamia utengenezaji wa kalavat kwenye mfereji husika kuepusha ajali kwa watoto wa polisi wanaoishi maeneo ya Themi Magharibi karibu na chanzo cha mfereji huo ulioleta utata jambo ambalo limekwisha shughulikiwa.
Aidha mwanachi mmoja amabaye hakutaka jina lake litajwe
wakati akihojiana na mwandishi wetu alisema kuwa wananchi wa Arusha wanajua
Rais ni Lowassa, Mbunge ni Lema na Diwani wa Themi ni Melance Kinabo, hakuna
asiyejua ufanisi na umakini wake wa utendaji, niseme tu viongozi hawa ni
wawajibikaji, wazalendo na watu makini.
Hivi ni moja ya vipaumbele vya Mh. Kinabo katika ahadi zake
iwapo wananchi watampa ridhaa tena ya kuwaongoza na kuwa Diwani wa kata ya
Themi mwaka 2015-2020.
- AFYA
Kujenga uzio na kukamilisha maboresho yote ya kituo cha Afya
Themi, ikiwemo ujenzi na ufungaji mashine ya kuchoma taka za Hospitali, ujenzi
wa chumba cha upasuaji kina mama wajawazito, na ununuzi wa Gari la wagonjwa
(Ambulance).
- MIUNDOMBINU NA MIPANGO MIJI
Upatikanaji wa
maeneo ya wazi kwajili ya biashara za vijana na akinamama. Kupata upimaji wa
maeneo mbalimbali ndani ya kata ( Mtaa wa Kambarage), ukarabati na ujenzi wa
barabara zote za kata, ikiwemo Serengeti (mtaa Corridor area, pamojana Engira
road, na Barabara za AICC Flats), kufungua barabara zinazounganisha kati ya
mtaa kwa mtaa na kata kwa kata. kuongeza nguvu za kisheria katika kuimarisha na
kuboresha miundombinu ya AICC barabara na nyumba, pia upatikanaji wa maji
safi na salama kwa uhakika, mfano mtaa wa AICC, Themi mashariki na
Kambarage. Aidha kujenga, na kutetea kwa nguvu zote hoja ya ukarabati wa
nyumba za polisi (Old polisi fire) chombo ambacho ni muhimu sana kwa raia na
mali zao.
- ELIMU
Jinsi ya kumsaidia Mtanzania ni kumpa Elimu. Alisema
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Cristopher Kongoye alipokuwa akimshukuru Mh.
Diwani wa Themi Melance Edmund Kinabo na kuungana nae kwa kusema, tunawaitaji
watu wanaoleta maendelea kama wewe na kumwaidi kumpa ushirikiano wa kutosha na
kusema hataitaji watu mizigo kwenye maendeleo.
Kwakutambua hilo, Mh. Kinabo ameongeza msimamo wake na
kuahidi kusimamia upatikanajii wa shule ya ufundi kwaajili ya vijana katika
shule ya msingi Engira.
Ufuatiliaji na usimamizi thabiti ili kupatikana kwa eneo la
ujenzi wa shule ya msingi kati ya kata ya Engutoto na Mtaa wa kambarage.
Ujenzi wa ukuta wa shule ya msingi Engira pamoja na
kukamilisha ujenzi na ukarabati wa Shule ya sekondari Themi na shule ya msingi
Themi.
- UCHUMI
Kuwezesha vikundi vya VICOBA kuwa SACCOSS
Kuanzisha/ kuunda kongamano la mafunzo kwaajili ya vijana
(Ujasiriamali)
Kutambua makundi maalum na kuweza kuwasaidia
Kuunda timu ya soka kata ya Themi.
- ULINZI NA USALAMA
Kuhakikisha kuwa vinaundwa vikundi vya vijana kwaajili ya
ulinzi shirikishi, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ndani
ya kata ya Themi.
No comments:
Post a Comment