Visa vya
ufyatulianaji wa risasi Bujumbura vimeongezeka tangu kutekelezwa kwa
jaribio la kupindua serikali miezi kadha iliyopitaWatu saba wameuawa
katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia kinachodaiwa kuwa jaribio
la wizi katika benki moja.
Majambazi sita waliuawa na polisi baada ya gari walilotaka kutumia kutoroka kuzuiwa na polisi, polisi wamesema.
Majambazi hao walikuwa wameua afisa mmoja wa polisi awali.
Mwandishi
wa BBC mjini humo Prime Ndikumagenge anasema ameona miili mitatu ikiwa
katikati mwa barabara na mingine miwili katika kituo cha mafuta
kilichoko karibu.
Mwili mwingine ulikuwa mita chache kutoka eneo hilo.BBC
No comments:
Post a Comment