Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari
Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12
kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku
wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.
Mtikila alitangaza kugombea Urais kupitia chama chake cha DP lakini
chama chake ni moja ya vyama ambavyo vilikatwa kutokana na kutotimiza masharti ya uchaguzi.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi.
No comments:
Post a Comment