Ni sikuchache baada ya uchaguzi mkuu, uliofanyika siku ya jumapili
tarehe 25/ October 2015 ambapo wakazi wa Themi walikuwa na wajibu mkubwa
sana wakuchagua kiongozi bora, mtendaji na mwenye kiu ya kufanya kazi.
Kata ya Themi ilikuwa ikiwaniwa na wagombea watatu wa vyama vya
CHADEMA, CCM na ACT wazalendo, ambapo Mhe. Melance Kinabo (Kaburu) wa
CHADEMA alitangazwa kuwa diwani mteule wa kata ya Themi baada ya
kushinda kwa zaidi ya asilimia 60 dhidi ya wagombea wengine waliokuwa
wakigombea kiti hicho cha udiwani.
Aidha Mhe. Diwani amewashukuru sana wananchi wa kata ya Themi kwa kumpa
tena ridhaa ya kuwaongoza kwa mara nyingine, akizunguza na chombo chetu
cha habari amesema "Nimekuwa diwani kwa muda mfupi sana, lakini utendaji
kazi wangu umenipa fursa ya kukubalika na wananchi, na hii ninawaahidi
kuwa nitawajibika kipindi hiki zaidi kuliko hapo awali" alisema.
mwananchi mmoja amabaye alijitambulisha kwa jina la ndg. Upendo
kassariwa amesema kuwa "Mh. Kinabo hakuwa na mpinzania, isipokuwa kuwepo
kwa vyama vingine ilikuwa ni sehemu tu ya vyama vingine kutaka tu
kuwapa changamoto wananchi na kumjenga kisiasa Diwani wetu, maana
walimtusi sana, walimkejeli lakini kutokana na kujitambua kwake na
kutambua heshima yake kwa wananchi yeye aliwajibika kusema sera makini
na kutangaza amani kipindi chote cha kampeni" alisema.
Mhe. Kinabo alimalizia kusema "Ninatambua matatizo ya kata yangu,
natambua uhitaji wa wananchi wangu, kwa heshima kubwa nina waambia kuwa
nitahakikisha ninatimiza ahadi zangu na kufanya yote kwa kumtanguliza
kwanza Mungu. ninawaomba ushirikiano wao pale nitakapo uhitaji kwa
maendeleo endelevu ya kata yetu, hususa katika maswala nyeti kama vile
ulinzi wa mali zetu, miundo mbinu n.k"
No comments:
Post a Comment