Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha manaibu katibu
wawili wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika
ikulu jijini Dar es Salaam.Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu
Emmanuel Kalobelo anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano
Sayansi na Teknolojia na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu
Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete leo.
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliapishwa keo.Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda.
No comments:
Post a Comment