CHAMA CHA MAPINDUZI kimeweka masharti au vigezo 13 ambavyo kila mtangaza nia kupitia chama cha mapinduzi ni lazima ajipime kwa vigezo hivyo ndipo aingie uwanjani.
1. Uwezo wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu alionaokatika uongozi wa shughuli za Serikali, umma na taasisi.
Hapa lazima mgombea awe na uzoefu na mambo ya utawala serikalini au Taasisi za umma.
2. UADILIFU,HEKIMA NA BUSARA
Mtangaza nia lazima awe ni mwadilifu,mwenye hekima na busara
3. AWE NA ELIMU YA CHUO KIKUU AU INAYOLINGANA NA HIYO
4. AWE NA UPEO NA UWEZO WA KUDUMISHA MUUNGANO,KUIMARISHA UMOJA NA KUENDELEZA AMANI NA UTULIVU.
5. UWEZO WA KUONA MBALI,KUTOYUMBISHWA NA KUWA NA MAAMUZI YA BUSARA KUHUSU MASWALA NYETI YA TAIFA
6. Awe na upeo mkubwa usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifaili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa jumla.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteka au ufashisti bali aheshimu na kuilinda Katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na taratibu za utawala bora.
8. Awe mtetezi wa wanyonge, kusimamia haki za binadamu, mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wake binafsi.
9. Awe mstari wa mbele kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza Sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi,
10. Awe mpenda haki na jasiri wa kupambana na dhuluma,maovu yote nchini,
11. Asitumie nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na wananchi
13. Awe makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa uongozi, watendaji, asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na ufanisi.

No comments:
Post a Comment