Sugu na mzazi mwenzake Faiza Ally pamoja na mtoto wao enzi walipokuwa pamoja.
Jana ilikuwa siku ya aina yake kwa msanii Faiza Ally na mzazi mwenzake,
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Wakati Faiza akimwaga
chozi katika chumba cha habari katika gazeti la Mwananchi alipofika
kutoa ujumbe wa kuomba radhi kutokana na vazi la kitenge lenye
kambakamba alilovaa siku ya Tamasha la Tuzo za Muziki za Kilimanjaro,
Sugu alimwaga chozi bungeni Dodoma alipowataka wabunge wasijadili mambo
yake ya faragha.
Faiza akiwa amevalia baibui na kufunika kichwa kwa hijabu, alieleza kwamba anajutia kutokana na kuvaa vazi lililoonyesha sehemu kubwa ya makalio yake alilodhani ulikuwa ubunifu. Mrejesho alioupata kuzomewa na jamii na picha zake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii aligundua amefanya kosa.
Pigo la pili, ambalo limemjeruhi vibaya moyoni ni mzazi mwenzake, Sugu kufungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo ya Sinza iliyompa haki ya kukaa na mtoto wao kwa madai mama yake kukosa maadili.
Hivi sasa Faiza anaona dunia imemwelemea anajuta na ameapa kutorudia tena kosa hilo. “Siwezi kurudia kosa, nitakuwa makini zaidi katika mavazi yangu,” alisema msanii huyo, huku akitokwa machozi alipozungumza jana na mwandishi wa habari hizi kwenye ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata Relini, Dar es Salaam.
Mwanadada huyo aliyewahi kuwa mrembo wa Tabata namba tatu katika mashindano ya mwaka 2005 na ambaye hujishughulisha na utayarishaji filamu, aliomba radhi kwa jamii kutokana na utovu wa maadili aliouonyesha siku ya tuzo hizo na bado anaomba wamsamehe.
“Wasanii wengi ni wabunifu na hufanya mambo kwa nia ya kufurahisha mashabiki kama ambavyo amekuwa akifanya Joti kuvaa nguo za kike na kupaka rangi ya mdomo, hivyo mavazi yangu yalikuwa na lengo la kutoka tofauti mbele za mashabiki wangu, lakini kwa yaliyonikuta hasa kwenye vazi la Kili niliomba msamaha kwa jamii na bado naomba wanisamehe,” alisema Faiza.
Hata hivyo, hilo la mzazi mwenzake kupewa haki ya kisheria na mahakama kumchukua mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili na miezi minane, kwa madai kadhaa ikiwamo ya uvaaji usiokuwa na staha, ni jeraha kubwa lililomfanya apite kwenye vyombo vya habari kupaza sauti ya kuomba radhi.
Sakata hilo pia limetua bungeni na baadhi ya wabunge wanawake walimlaumu Sugu wakidai kampora mtoto mzazi mwenzake kwa vile ni mnyonge, lakini jana mbunge huyo, aliyewahi kutamba nchini na muziki wa Hip Hop alitoa ufafanuzi wa kina na kuwataka wabunge wasiingilie maisha yake ya faragha.
“Wabunge tuliomo humu ndani, baadhi wametumia madaraka yao vibaya katika kuwanyanyasa wanawake. Ninasema haya kwa sababu nina ushahidi. Tuna mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu, ameenda kutumia siku moja mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili, kitu ambacho kwa kweli wanaume waangalie namna ya kuwaenzi na kuwaheshimu wanawake hasa katika suala la kulea watoto. Ni mbunge kutoka Chadema kama Chadema wanathamini utu wa mwanamke wangemshauri mbunge mwenzao,” alisema juzi mbunge wa viti maalumu (CCM), Martha Mlata.
Hata hivyo, jana Sugu alijibu kwa uzito akieleza taratibu alizotumia kufungua kesi mahakamani, uamuzi ulivyotolewa na namna alivyomwacha kwanza mtoto kwa mama yake yafanyike majadiliano ya kifamilia.
“Kwa taarifa tu pamoja na mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu, nimetoa nafasi ili majadiliano ya kifamilia yafanyike. Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa,” alisema Sugu ambaye alionekana akifuta machozi akisikitishwa suala hilo kuzua mjadala bungeni.
Majibu ya Sugu
Akitoa ufafanuzi katika kikao kilichosimamiwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM) Sugu alisema, “Naomba nitoe maelezo binafsi. Jana (juzi) tarehe 25 Juni 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa Chadema amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake,” alisema Mbilinyi.
Alisema ingawa Mlata hakutaja jina la mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake na alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. “Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi. Mimi ndiye baba wa mtoto anayedaiwa kuporwa kwa mama yake. Na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa mtoto wetu,” alisema Sugu.
“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani. Nadhani sitakosea kusema hata Mlata mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika. Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndiyo maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu,” alisema.
Sugu alilieleza Bunge kuwa mtoto ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012. Katika kipindi chote amekuwa akimpelekea mama yake Sh500,000 kila mwezi, pia anamlipia ada ya shule Sh3 milioni kila mwaka.
“Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika mitandao ya kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi. Picha zake nyingine akiwa amevaa ‘diapers’ zilisambaa mitandaoni na Mlata anayejulikana kuwa ni mlokole angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge,” alisema.
Kutokana na mazingira hayo Sugu alisema kwamba alilazimika kwenda Mahakama ya Mwanzo Manzese, kuwashilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzake asingeweza kumlea mtoto kwa maadili yafaayo, ambapo aliitwa akajitetea, Juni 23 na mahakama iliridhika na ushahidi wake, ikaamua akabidhiwe mtoto ili amlee.
“Kwa taarifa tu pamoja na mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu, nimetoa nafasi ili majadiliano ya kifamilia yafanyike. Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa,” alisema mbunge huyo, ombi ambalo Ndugai aliafiki.
Maelezo ya Faiza
Uamuzi wa kesi hiyo uliotolewa Juni 23 mwaka huu umesababisha maumivu makubwa kwa mrembo Faiza ambaye licha ya kuchukua hatua ya kuukatia rufaa, anajuta na kuapa kutorudia tena kuvaa mavazi ya mitindo hilo pamoja na kwamba ameizoea.
Faiza akiwa ameongozana na kaka yake aitwaye Abdulaziz Ally, alifika katika ofisi za gazeti hili, kuelezea jinsi alivyojikuta kwenye wakati mgumu katika hali ambayo hakuitarajia maishani mwake, ikichangiwa na mitindo ya mavazi yake aliyoyaita kuwa ni ya kisanii.
“Hakika nimejikuta kwenye wakati mgumu na sivyo ambavyo baadhi ya watu wanafikiri. Hali hiyo ilinitokea nikiwa kule kule kwenye Kilimanjaro Music Award tena baada ya kubaini picha zinazoonyesha makalio yangu zimewekwa kwenye mitandao. Niliamua kuondoka haraka katika eneo hilo, kabla ya muda niliyokusudia,” alisema Faiza.
“Ingawa nimezoea kuvaa nguo fupi lakini sikupanga kuonyesha makalio, bahati mbaya ni kwamba ile nguo nilipoivaa awali kabla ya kuondoka nyumbani ilikuwa imekaa vyema. Nafikiri baada ya kukaa kwenye gari ilifumuka bila mimi kujua, hadi nafika ukumbini na kuingia pale kwenye zulia jekundu natembea kumbe huko nyuma mapaparazi wanapiga picha. Hakuna hata aliyenishtua,” alisema.
Faiza alisema kutoka na kujiona kwenye mitandao ya kujamii alijisikia vibaya na kutamani angekuwa mmiliki ili azifute zile picha kwa sababu zilionwa hata na watu ambao hawakustahili, hivyo kumjengea taswira mbaya ambayo hakuitarajia.
Kuhusu jinsi alivyoamua kuvaa ‘pampers’, alisema kuwa alivaa hivyo kama msanii na hakuna na shaka nalo kwa kuwa urefu ulikuwa sawa na kaputura fupi ambazo amekuwa akivaa. Hata siku alipovaa shati pekee, alisema nalo lilikuwa na urefu sawa na magauni au sketi za vimini.
“Napenda kuweka wazi naumizwa na watu ambao wanaendelea kusambaza hizo picha za makalio, watambue tu leo imenifika mimi lakini siku nyingine itawafika na wao maana sisi sote ni binadamu, tunafanya makosa kwa nyakati tofauti,” alisema huku akifuta machozi.
Aidha, amewashukuru wote ambao wamkuwa wakimtetea kwa namna moja au nyingine kwa kuwa wamekuwa faraja kwake, tofauti na wale wanaomkashfu, wanamuumiza na kama angekuwa na moyo mwepesi angechukua uamuzi mbaya.
“Namshukuru Mungu nimeweza kuhimili hali hii kwa kiasi fulani, maana naamini mtu mwingine angeweza hata kuamua kuwa mlevi au kuwa mbaya lakini nashukuru nina uamuzi wa kubadilika, nampenda mwanangu sitaki kuwa mbali naye,” anasema.
-Mwananchi

No comments:
Post a Comment