Wageni wa Makongoro Nyerere waliotoka Visiwani Zanzibar.
Mbunge wa Afrika Mahariki Makongoro Nyerere akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa fomu katika ukumbi wa CCM Dodoma leo.
Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere pamoja na Balozi Amina Salum Ali leo wamechukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika kinyanga’anyiro kitachofikia tamati mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu hiyo ya Urais Makongoro Nyerere amesema kwamba akipata nafasi ya kuwa rais wa Tanzania ata hakikisha kuwa ana pambana na ufisadi pamoja na mafisadi kwa kuwa serikali imeshindwa kuwashughulikia kwa kuwa na majina makubwa serikalini.
'Tanzania ni tajira sana, ina pesa nyingi, wanafunzi hawapaswi kukosa mikopo hasa watoto wa maskini madaktari hawapaswi kumwangalia mgonjwa wakamwacha na kuondoka kwa kumliwaza kwa maneno, polisi hawatakiwi kuwa na filimbi na bangi mfukoni ili kukamata watu waje kukombolewa, mahakama za chini, mahakimu wakihongwa kuku wanaweza kuhukumu hata wake zao kwa njaa walizokuwa nazo, wakurugenzi wanapigiwa simu watoe hela usipotoa unahamishwa kwa sababu tu ya makundi ya uraisi ndani ya chama, pesa hazifiki kwa hawa wafanyakazi, sasa wamezigeuza majina sasa zinaitwa EPA, ESCROW, RICHMOND, na DOWANS. Vibaka wanagawana, ifahamike kuwa CCM sio chama cha wala rushwa, hawa watu wachache kwanini wakichukue chama chetu, wakipeke wapi, na watuache sisi wapi, tunakitaka chama chetu cha wakulima na wafanyakazi.
Ndugu watanzania sipotayari kuwaiga hao kwakusema "nikishindwa ama kukosa ridhaa hii, patachimbikah uko nikutaka kutitia wote, kuchimbika huku hakutokei kwingine popote isipokuwa kwa watanzania wote"
Kwa upande wake Amina Salum amesema kwamba anaomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi huku kauli mbiu yake ni matumaini mapya kwa kizazi kipya na kuahidi kutowaangusha watanzania kwani wanawake wamekuwa na historia ya kutohusika na ufisadi pamoja na utendaji wenye tija.
Leo wanasiasa wanne wamechukua fomu ya kugombea urais ambapo ratiba inaendelea tena siku ya kesho kwa wanasiasa takribani watano wengine kuchukua fomu.
No comments:
Post a Comment