Mwaka
1997 Watanzania waliambiwa dhahabu ndio mwarobaini wa umasikini. Mwaka
2015 Watanzania wanaambiwa Gesi Asilia ndio mwarobaini, Nchi kama
Nigeria, Angola, Equatorial Guinea nazo zina utajiri mkubwa wa mafuta na
gesi. swali Je, vyote hivi vimeweza kuwa suluhisho la umasikini katika
nchi zao?
Karibia
wagombea wote wa CCM waliojitokeza hadi sasa hakuna aliyehusika kusema
anamikakati gani ya kuhakikisha analeta chachu ya maendeleo katika
kufufua viwanda vilivyo poteza fursa za maelfu ya ajira, na ongezeko la
uchumi wetu.
rushwa sio sababu pekee ya
kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania, na wala sio sababu ya kutokuwepo
kwa fursa za ajira sekta ambayo inauwezo wa kutengeneza uchumi wetu
kukua na kushika kasi katika nchi zinazo kuwa kiuchumi duniani.
No comments:
Post a Comment