SERIKALI imewashauri Waandishi wa Habari nchini kuchagua na kubobea katika sekta mbalimbali maalum ili kuinua kiwango cha taaluma ya habari na kuwapa wananchi taarifa muhimu kwa umakini zaidi katika nyanja husika ili kuleta maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juma Nkamia alipokuwa akijibu swali la msingi la Mhe. Haroub Shamis, Mbunge wa Chonga.
"Serikali imekuwa ikiweka msisitizo kwa Vyuo vya Uandishi wa Habari kutayarisha mitaala yao ili kuwawezesha Waandishi wa Habari kubobea kwenye Sekta muhimu zikiwemo Uchumi, Afya, Mawasiliano, Mazingira na zinginezo,"alisema Mhe.Nkamia.(P.T)
Mhe. Nkamia amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Waandishi wa Habari nchini katika kutoa Habari, Kuelimisha na Kuiburudisha jamii,pia mchango huu wa waandishi umesaidia katika kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na hata maendeleo ya taifa.
Aidha Mhe. Nkamia amesema Serikali imekuwa ikihakikisha kuwa Waandishi wa Habari wanatekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa imekuwa ikiridhia uanzishwaji wa vyama vya kitaaluma ambavyo huandika habari zilizobobea katika Sekta maalum.
Vyama vya kitaaluma ambavyo serikali iliridhia kuanzishwa kwake ni pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari za Bunge, Ukimwi (AJAAT), Uchumi, Mazingira (JET).
Vyama vingine ni Chama cha Waandishi wa Kodi (TEWNET), Michezo (TASWA), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO)
No comments:
Post a Comment