Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wahasibu wakuu nchini kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha kwamba zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete wakati akifungua mkutano wa 22 wa siku nne wa Wahasibu Wakuu wa Serikali wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG)unaendelea katika ukumbi wa wa mikutano wa Kimataifa Mwalimu Julius K. Nyerere uliopo jijini Dares Salaam.
“Wakati mwingine ripoti zinaandikwa vizuri, lakini si halisi, ukichunguza utakuta fedha zimetumika na hakuna kilichotekelezwa,” alisema Rais Kikwete huku akitolea mfano wa halimashauri moja ambayo ripoti yake ilionesha kuwa fedha kadhaa zilitumika kujenga shule na nyingine madaraja mawili yamejengwa wakati hakuna kilichojengwa,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete aliwataka wahasibu hao, kuhakikisha rasimali za nchi zinatumika kulingana na mahitaji yaliyokusudiwa.
Alisema zaidi ya asilimia 70 ya fedha za Serikali zinatumika katika sekta ya manunuzi ,hivyo aliwataka wahasibu hao kuendelea kudhibiti suala hilo ili kuepusha kuwepo kwa mianya ya rushwa.
Rais Kikwete aliongeza kuwa wakati alipoingia madarakani makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa sh.bilioni 170 kwa mwezi sasa yamefikia bilioni 900 hivyo hali hiyo imetokana na jitihada za maboresho mbalimbali.
Aliongeza kwamba Tanzania itaendelea kuboresha usimamizi wa matumizi ya fedha za umma kwa uwazi na uwajibikaji .
Kwa upande wake Waziri wa Fedha Saada Salum Mkunya alisema mkutano huo utasaidia wahasibu hao kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa taaluma hiyo.
Alisema kupitia ESSAG Tanzania imeweza kunufaika kwa kuiwezesha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanyakazi kwa huru zaidi, pia baadhi ya wanataaluma wa fani hiyo wamepatiwa mafunzo.
No comments:
Post a Comment