TTCL

EQUITY

Wednesday, March 18, 2015

Fid Q apewa Tuzo Na Umoja Wa Nchi Za Ulaya EU


Fid Q apewa tuzo na umoja wa nchi za ulaya EU, ‘CHAMPION of the 2015 European year for development in Tanzania
Umoja wa nchi za ulaya EU wamempa rapper Fareed “Fid Q” Kubanda tuzo ya ‘CHAMPION of the 2015 European year for development in Tanzania’ kutokana na mchango wake katika jamii.
“Tarehe hii ya leo ambayo ni 17 machi ikiwa siku ya Jumanne […] nina furaha sana kwasababu ni siku ambayo nimepewa tuzo…tuzo hii inaitwa ya CHAMPION of the 2015 European year for development” alisema Fid Q kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.
Fid ameelezea sababu iliyowafanya EU kumpa tuzo hiyo.


“Lakini nimepewa kwasababu gani? wamesema kwamba kwasababu maisha yangu yana ‘exemplify’ uhalisia wa maisha ya wengine kwa jinsi ambavyo nimetenga muda wangu kusaidiana na jamii. Kwahivyo hivi ni vitu ambavyo wao wameviona wakaona kwamba hapana wanakila sababu ya kuonesha kwamba wameuona na kuutambua na kuthamini mchango wangu.”

Fid ameongeza kuwa anampango wa kulirudisha darasa la Ujamaa Hip Hop ambalo alikuwa akitoa elimu kwa vijana mbalimbali wa mitaani na wengineo wanaojihusisha na mihadarati, na hiyo ni moja ya michango aliyoitoa kwa jamii iliyofanya apate tuzo hiyo.

No comments:

Post a Comment