Mkurugezi wa kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Jerusalem Films, Jacob Stephen ‘JB’ambae pia ni muigizaji na muongozaji wa filamu, amewaeleza mashabiki wake kuwa wakae mkao wa kula kwani baada ya wiki iliyopita kuingiza movie ya Mzee wa Swaga sokoni, sasa hivi wapo katika maandalizi ya kutoa movie nyingine mwezi ujao.
"Asanteni sana wadau wa Jerusalem films kwa kuipokea vyema Mzee wa Swaga. sasa tunajiandaa kuwaletea movie nyingine inaitwa CHARLE MVUVI : Waigizaji:Hadji Adam,Shamsa Ford,Mzee Halikuni na Makombora wote wa zanzibar.Movie hii imechezwa zanzibari na inatarajiwa kutoka mwezi ujao". JB aliaeza.
Haya jamani tukae mkao huo basi!!
No comments:
Post a Comment