MSANII wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Farhad wanadaiwa kumwagana baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Nisha na mpenzi wake huyo ambaye walikuwa na mipango ya kuoana mwaka jana lakini ndoa ikayeyuka waliachana kutokana na sababu zisizojulikana na sasa kila mmoja yupo bize na maisha yake.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Nisha ili kuzungumzia habari hizo ambapo alikiri kwamba ni kweli wamemwagana.“Sababu za kuachana siwezi kuziweka wazi kwa sasa, niko kikazi zaidi mambo ya mapenzi nimeyaweka pembeni nataka nitimize malengo yangu ambayo hayakutimia mwaka jana,” alisema Nisha.
No comments:
Post a Comment