TTCL

EQUITY

Tuesday, January 13, 2015

SOKA LETU: MCHEZAJI WA KIKE ADHANIWA KUWA MWANAUME

genoveva

Kumekuwa na vitendo kadhaa vya kuwatilia mashaka wanamichezo wa kike hasa pale wanapokuwa na uwezo mkubwa kuliko kawaida na mashaka zaidi hutiliwa kwenye uhalisia wa jinsi zao ambapo wengi huhofiwa kuwa si wanawake halisi bali ni wanaume .
Hii iliwahi kumkuta mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya na safari hii imemkuta mwanasoka toka Nigeria Genoveva Anonma ambaye katika hali ya kuhuzunisha alidhaniwa kuwa mwanaume .
Mbaya zaidi ni kwamba Genoveva alikutana na kadhia hii toka kwa Waafrika wenzie ambao ni viongozi wa mamlaka kuu za soka Afrika ambao walidhani binti huyu anadanganya kuhusu jinsia yake ya kike .
Viongozi wa timu za Ghana , Nigeria na Afrika Kusini walidhani Genoveva Anonma ni mwanaume.
Viongozi wa timu za Ghana , Nigeria na Afrika Kusini walidhani Genoveva Anonma ni mwanaume.
Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea  alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa ili kuthibitisha kuwa ni msichana na si mvulana kama ilivyokuwa inahofiwa nah ii ni kutokana na nguvu ambazo anazo akiwa uwanjani na ubora alioonyesha .
Genoveva akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa alidhani kuwa uthibitisho wa insi hufanywa hospitalini na alidhani angeitwa hospitalini lakini cha kushangaza ni kwamba alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa jambo ambalo anakiri kuwa lilimsababishia fedheha na hasira.
Genoveva Anonma alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa jinsia yake .
Genoveva Anonma alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa jinsia yake .
Kashfa hii ilianzishw akwenye muichuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kina mama ambapo viongozi wa Ghana , Nigeria na Afrika Kusini walizusha hoja kuwa wachezjai watatu wa Equatorial Guinea ni wanaume na si wanawake .
Hofu hii iliondolewa baada ya wachezaji hawa kiukaguliwa na kugundulika kuwa wanawake halisi .
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amewahi kuhisiwa kuwa mwanaume .
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amewahi kuhisiwa kuwa mwanaume .

No comments:

Post a Comment