MWIGIZAJI na Mchekeshaji Bongo, Griady Kahena ‘Masai Nyotambofu’ amefunguka sababu zilizomfanya apumzike kuigiza katika Kundi la Vituko Show kuwa ni bosi wake kutowajali wasanii hasa wakiwa na shida.
“Ukiangalia Vituko Show sisi magwiji tulioanza na kundi hilo, wengi tumekimbia baada ya kuona bosi haoni umuhimu wetu pamoja na kufanya kazi lakini unaambulia maarufu tu huna pesa, una shida unaazima hata simu,” anasema Nyotambofu.
Nyotambofu ambaye kwa sasa ni mtangazaji katika kipindi cha MinBazz kirukacho katika televisheni ya Star Tv. Msanii huyo amebainisha kuwa kufuatia utaratibu wa bosi wao kuwachukulia kama wasanii wa kawaida, wengi wamejitoa na kuangalia kazi nyingine badala ya kuigiza ili kuweza kuendesha maisha yako.
No comments:
Post a Comment