Tanzania yaadhimisha miaka 20 ya sekta ya utangazaji huria ambapo imesema kuwa kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta hiyo nchini Tanzania.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara
Serikali imeviagiza vyombo vya utangazaji nchini kuhakikisha watangazaji wao wanapatiwa mafunzo na kupewa ujuzi wa kufanya kazi kwa uadilifu kwani ubora wa vipindi na maudhui yanayotangazwa yanategemea ni kwa kaisi gani wamiliki wamewekeza kwa watangazaji wao.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara wakati akifungua mkutano wa mwaka ulioambatana na kusherehekea miaka 20 ya sekta ya utangazaji huria ambapo amesema kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta hiyo na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha maudhui bora yanatolewa kwa watazamaji na wasikilizaji.
Mkurugenzi mkuu wa TCRA Prof John Nkoma amesema licha ya Tanzania kuhamia dijitali jambo ambalo limeongeza wigo kwa msikilizaji na mtazamaji, bado kuna changamoto kwenye maudhui ya ndani yanayoendana na utamaduni wa mtanzania na kwamba miaka 20 tangu sekta ya utangazaji kwa watu binafsi iruhusiwe kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya namna ya uwasilishaji maudhui.
Naye mwenyekiti wa kamati ya maudhui wa TCRA Mhandisi Margtreth Munyangi amesema wakati umefika serikali kuhakikisha inakuwa na baraza la habari ambalo mbali na kusimamia maslahi ya waandishi litasimamia taaluma yenyewe kama ilivyo katika sekta nyingine.
No comments:
Post a Comment