Waombolezaji wakiwa msibani.
Morogoro: Mwimbaji maarufu wa nyimbo za lnjili Bongo, Rose Muhando ameshindwa kuhudhuria mazishi ya dada yake wa damu, jambo lililowakera baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki.
TUJIUNGE KIJIJI CHA MAGOLE
Ishu hiyo ilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa wazazi wa staa huyo katika Kijiji cha Magole, Dumila wilayani Kilosa mkoani hapa ambapo dada wa tumbo moja (toka, nitoke) wa Rose aitwaye Shida Athuman Muhando alifariki dunia ghafla.
Ndugu na jamaa wa marehemu dada yake Rose Muhando
wakilia kwa uchungu.
Mwandishi wetu ambaye alifika kijijini hapo, alielezwa kwamba Shida alikuwa akitibiwa katika Zahanati ya Roma iliyopo Dumila (ugonjwa haukutajwa) ambapo Rose alipewa taarifa lakini hakufika.
Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa marehemu Shida na mjomba mkubwa wa marehemu, Mohamed Seif Matambo, Rose alipewa taarifa juu ya kifo hicho lakini hadi mazishi yanafanyika hakufika na alipopigiwa simu, muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa kumpa pole hakujibu.
Marehemu dada wa Rose Muhando, Shida
Athuman Muhando enzi za uhai wake.
“Rose anayejifanya ana fedha, hataki hata kuzika ndugu zake,” alifoka mmoja wa vijana waliohudhuria mazishi hayo aliyejulikana kwa jina moja la Kesi na kuongeza:
“Rose ni dada yetu wa damu, juzikati alifariki dunia Semeni (mtoto wa dada wa Rose) hakuja kuzika, sasa amefariki dunia Shida.
ROSE ASIKITIKA
“Tulimpigia simu akasikitika sana, akasema anakuja. Siku mbili mfululizo tumempigia na kumtumia ujumbe mfupi (SMS) hadi sasa ni saa 10:00 jioni. “Anajua kabisa kwamba tunamsubiri yeye kwa kuwa ndiye aliyeachiwa familia lakini kinachoonekana ametususia. Tunasikia yupo Dar. Tumeona muda unayoyoma tukawaambia mashehe tumpumzishe marehemu kwani mtu mwenyewe hatujui kama atakuja.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za lnjili Bongo, Rose Muhando.
KUMBE NI MKRISTO PEKEE
“Katika familia hii, yeye pekee ndiye Mkristo hivyo kinachoonekana anataka kujitenga na sisi kwani alianza muda mrefu.
ROSE VIPI?
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Rose kwa lengo la kutaka kujua sababu zilizomfanya ashindwe kwenda kwenye msiba wa dada yake lakini simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS za kumwaga hakujibu.
No comments:
Post a Comment