Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani limeendelea kushirikiana na wadau wengine wakiwemo chama cha msalaba mwekundu katika kuhakikisha linapambana na matukio ya ajali za barabarani
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani limeendelea kushirikiana na wadau wengine wakiwemo chama cha msalaba mwekundu katika kuhakikisha linapambana na matukio ya ajali zinazoendelea kutokea nchi nzima sambamaba na kutoa huduma ya kwanza kwa waathirika wa ajali hizo hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kamanda Mohamed Mpinga amesema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali katika jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine huku sababu kubwa ya ajali hizo ikiwa ni uzembe wa madereva kutofuata sheria za barabarani na kubaini toka operesheni ya ukaguzi wa magari na madereva kuanzishwa nchi nzima kumekuwepo na mafanikio makubwa.
Baadhi ya wadau wanaoendelea kushirikiana na jeshi hilo wakiwemo chama cha msalaba mwekundu, wamebaini wametoa wito kwa madereva kuwa makini na kufuta sheria za barabarani ili kuhakikisha ajali hizo zinapungua na hatimaye kuisha kabisa.
Wakati kikosi hicho kikiendelea na ukaguzi wa kukamata magari na madereva wanaovunja sheria EATV imeshuhudia dereva wa bodaboda na bajaji wakisababisha ajali kwa kufanyiana ubabe kitendo kilichoelezewa kuwa cha uzembe kwa madereva wote wawili.
No comments:
Post a Comment