Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya kwa kushirikiana Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wawili kwa kula njama na kuwakeketa watoto wanne kike wanne wakazi wa kijiji cha Marasibora mkoani Mara.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishina Msaidizi Lazaro Mambosasa akizungumza na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Mara.
Akizungumza baada ya watu hao wawili akiwemo mzazi na Ngariba kufikishwa kituo cha polisi cha Kinesi wilayani Rorya, Mratibu wa CCT wilayani humo Bw Isack Salasala, amesema baada ya CCT kupata taarifa kuhusu wanawake hao kuwafanyia ukatili watoto wa kike ambao wana umri chini ya miaka 14 walitoa taarifa polisi na kufanikishwa kukamatwa.
Kwa upande wake Ngariba mstaafu Bi Scholastika Kihore, amesema baada ya kupata elimu juu ya madhara ya vitendo hivyo vya ukeketaji alilazimika kuacha kazi na kujiunga na vikundi vya VICOBA kwa ajili ya kupata fedha za kuboresha maisha yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishina Msaidizi Lazaro Mambosasa, amesema mkoa wa Mara unasifika kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukiwemo ukeketaji watoto wa kike huku akitumia nafasi hiyo kuwataka Mangariba wote kujisalimisha kabla yakufanya kuanza msako mkali wa nyumba hadi nyumba.
No comments:
Post a Comment