Mtengeneza wa filamu mkongwe hapa nchini, William Mtitu ameendela kuwaponda baadhi ya wasanii ambao wanafanya kazi na kampuni ya Steps Entertainment kwa kukubali kushisha bei ya kazi zao kutoka shilingi 3000/= hadi shilingi 1,500 /= kwa CD moja kwa rejareja.
Kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM, Mtitu aliweka picha hiyo hapo juu na kuandika maneno haya;
"Wakati tukiangaika maporini kushuti sinema zenye ubora wasanii wenzetu sijui tuite upumbavu au kutojielewa wanajifungia ndani na wàhindi wao wawili eti wanataka kushusha bei sinema bei ya jumla iwe ziuzwe elfu moja (1,000/=)na rejàreja ziuzwe elfu moja na mia tano(1,500/=) hii nizi ni njama ili kuua wasambazaji wengine na ni dharau kubwa sana kwa wale wote waliotoa nguvu zao kwa hali na mali mpaka tasnia ya sinema imefika hapa ilipo,
kiukweli atuwezi kukubali hata kidogo na lazima tushinde hivi vita kwa gharama yeyote".
No comments:
Post a Comment