TTCL

EQUITY

Wednesday, December 24, 2014

JK AWAFUNGUKIO VIONGOZI MAFISADI

ATAKA WANAOKIUKA MAADILI KUWAJIBISHWA

Rais Jakaya Kikwete. 
RAIS Jakaya Kikwete amesema ni lazima watumishi wa umma wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma wawajibishwe ili iwe fundisho kwao na kwa wengine.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam juzi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kumkaribisha kuzungumza na wazee wa jiji hilo.

Awali kabla ya Rais kuzungumza, Sadiki katika hotuba yake alimwelezea Rais jinsi Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa ulivyofanyika jijini mwake na kusema CCM imefanya vizuri kwa kuibuka na ushindi wa jumla ya asilimia 75.

“Mheshimiwa Rais, katika ya mitaa 557 ya jiji hili, 555 ndiyo iliyofanya uchaguzi hiyo miwili haikufanya kwa sababu mbalimbali na matokeo ni kwamba CCM imeendelea kufanya vizuri tumepata ushindi wa jumla ya asilimia 75,” alisema Sadiki.

Na kuongeza Chadema ilipata asilimia 14, CUF wao walipata asilimia 11 na NCCR-Mageuzi wao walipata asilimia 0.1. Akizungumzia suala zima la uchaguzi huo nchini, Rais alivipongeza vyama vyote kwa ushiriki wao na wale walioshinda aliwashauri kutafuta mbinu za kuwakomboa wananchi waliowaamini na kuwapa kura.

Aidha, alipongeza uamuzi wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, Hawa Ghasia kwa kuchukua hatua dhidi ya watendaji wa umma waliosababisha kuwapo kwa kasoro kwenye baadhi ya maeneo katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini.

Rais alisema: ”Nampongeza Waziri Ghasia kwa kuchukua hatua na mimi namuunga mkono jambo hilo limetekelezwa kwa baraka zangu, aliniletea mapendekezo ya uamuzi wake huo na mimi niliandika ‘naunga mkono,’”alisema Rais Kikwete.

Alisema hivyo ndivyo inatakiwa kwa watumishi wa umma wanaozembea kazi kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma na kwamba kwa hatua hizo, ni wazi zitakuwa fundisho kwa wengine na hata kwenye uchaguzi mkuu ujao.

“Hili ni fundisho na tunataka wajue kwamba wenyewe wapo, na watawawajibisha na nimeongea na wakuu wa vyombo vya juu vya ulinzi wawawajibishe na wawatie nguvuni wavunjifu wa amani kwenye uchaguzi huo,” alisisitiza Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment