Wakati flani nilipoitembelea Afrika Kusini niliambiwa na mwenyeji wangu kwamba wizi wa magari unafanyika hata barabarani, unaweza ukawa umesimama kwenye mataa ukisubiri uruhusiwe lakini ghafla watakuja majambazi na silaha wanazuziba kwa mbele kisha wanachukua gari na kuondoka nalo.
So inaelekea wizi wa magari unaweza kuwa ‘kipaji’ kwa hawa ndugu zetu wa Afrika Kusini manake kuna kijana mmoja wa miaka 19 huko Northern Cape alifanya kitendo cha kujiamini zaidi pale alipoiba gari la Polisi, yaani ingekua ni gari binafsi linalomilikiwa na askari ingekua afadhali ila hili aliloiba ni gari la Polisi kabisa na nembo zake.
Ishu imetokea Jumamosi ya November 15 2014 na unaambiwa Polisi walianza kumsaka mtu huyu na kufanikiwa kumpata baadae yeye pamoja na gari ambapo baada ya kukamatwa alikua anatarajiwa kufikishwa Mahakamani Jumatatu ya November 17 2014.
Ilikuaje mpaka akafanikiwa kuliiba? ……alipata hiyo nafasi baada ya Polisi kwenda kwenye eneo la tukio kulikotokea ajali kwa hiyo baada ya Polisi wote kushuka huku funguo za gari zikiwa zimeachwa sehemu yake ndio jamaa akapiga gia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza.
No comments:
Post a Comment