Wazee nchini wameiitaka serikali kuchukua hatua za
kutofautisha siku ya sherehe ya uzimaji wa mwenge wa uhuru na
kumbukumbu ya kumuenzi baba wa taifa hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ili kuongeza uzito zaidi katika siku hiyo
muhimu ya kumuenzi muasisi huyo wa taifa la Tanzania.
Wakizungumza katika kongamano maalum la maadhimisho ya
miaka 15 ya kifo cha baba wa taifa hayati mwalimu Julius
Nyerere ambalo limefanyika eneo la mwitongo kijijini Butiama
mkoani mara, wawakilishi wa wazee hao kutoka mikoa ya
tanzania bara na visiwani,wamesema hakuna sababu ya kuchanganya
siku hiyo muhimu ya kumkumbuka muasisi wa taifa la tanzania
na shughuli za uzimaji wa mwenge wa uhuru.
Hata hivyo wazee hao wameonesha kuchukizwa na baadhi ya
viongozi wanaoshindwa kumuenzi mwalimu nyerere kwa kuchukizwa na
vitendo vya rushwa,ukiukwaji mkubwa wa maadili na miiko ya
uongozi kwa kusema kuwa viongozi wengi wamekuwa na tabia ya
ubinafsi na kujilimbikizia mali huku wakiwasahau watu
wanaowangoza.
akizungumza baada ya wazee hao kutoa tamko hilo,mmoja
watoto wa baba wa taifa Mh.Makongoro Nyerere, amesema wakati
watanzania wakiadhimisha miaka 15 bila mwalimu, kuna haja kwa
taifa kuandaa taratibu za kisheria zitakazosimamia maadili na
miiko ya uongozi ili kuwabana wahusika badala ya sasa
viongozi wengi wamekuwa wakitumia majukwaa ya kisiasa kwa
kudai kumuenzi kiongozi huyo.
Wazee hao pia wamepata fursa ya kuweka mashada ya maua
katika kaburi la baba wa taifa na kuungana na wakazi wa
butiama wakiongozwa na familia na baadhi ya viongozi wa
mkoa wa mkoa wa mara kushiriki katika misa maalum ya
kumuombea baba wa taifa hayati mwalimu julius nyerere kisha
kupanda miti katika msitu wa muhunda katika eneo la mwitongo.
No comments:
Post a Comment