TTCL

EQUITY

Thursday, December 26, 2013

BONGO FOLENI KWISHA..!! TAZAMA BASI ZITAZOLETWA ZENYE UWEZO WA KUTEMBEA KWENYE MAJI NA NCHI KAVU..!!


Kampuni ya Transevents Marketing Ltd kutoka Nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi ambayo kutoka Uholanzi  yanauwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayo anzia Tanzania kuwa na aina hiyo ya mabasi.


Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.

Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu.

Mchakato huo umekwisha anza kufanyiwa kazi pia kwa ushirikiano wa SUMATRA Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu na kazi pia kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.

Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania

Tazama Video la Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio

No comments:

Post a Comment