Timu
ya Kikapu ya Pistons imemtema Mchezaji wake kutoka nchini Tanzania,
Hasheem Thabeet ambaye amejiunga na Pistons mwezi septemba akitokea
klabu ya Philadelphia iliyokuwa imemchukua kutoka Oklahoma City Thunder.
Alicheza
dakika tano tu katika mchezo mmoja wa pre season na katika mwezi huu
amecheza dakika tano tu dhidi ya Washington Wizard huku akikosa jaribio
lake moja na kufunga.Pamoja na Hasheem Thabeet wengine waliofungasha virago ni Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic.
No comments:
Post a Comment