Shirika
la ndege la Australia linalofahamika kama Qantas limeanza kurusha ndege
yake ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi ya abiria duniani na inayofanya
safari zake kwa umbali mrefu zaidi.
Ndege
hiyo iliyotwa kama Airbus A380 ilitua katika uwanja wa kimataifa wa
Dallas-Fort Worth saa 15 tangu ilipoondoka Sydney, Australia safari ya
Kilometer 13,805 ikiwa na abiria 480 .
Uwanja
wa kimataifa wa Dallas- Fort Worth ni uwanja mkubwa wa ndege
unaounganisha ndege zote za Marekani na Latin America. Uwanja huo
umeonekana kufaa zaidi kwa ndege hiyo.
Angalia picha za ndani

No comments:
Post a Comment