KUNA TETESI ZINASEMA KUWA IPHONE 6,SIMU MPYA ILIYOTOKA HIVI KARIBUNI INAJIPINDA YENYEWEE
Wataalamu wana hisia mseto kuhusu ikiwa Apple inapaswa kujibu madai ya iPhone 6 kujipinda
Watafiti
wamechanganyikiwa kuhusu ikiwa kampuni ya Apple inapaswa kutoa kauli
yake kuhusu ripoti kuwa simu yake mpya ya iPhone 6 inajipinda mtumiaji
anapoishi kuiweka ndani ya mfuko wa suruale yake.
Watu
kadhaa ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao
kwenye mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa
na tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa 'Geek.com' pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na
haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi
wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya
Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa
za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za
kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the
Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.
Baadhi ya watu wameku wakituma picha za simu zao zilizojipinda
Russell Holly, anayefanyia kazi mtandao wa habari wa geek.com,ni mmoja wa wale walioripoti kuwa simu yake imejipinda.
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter, wametu moani yao kuhusu habari za simu hiyo kujipinda.
BBC ilijaribu kuwasiliana na Apple kuhusu ripoti hizo lakini haijasema chochote mpaka sasa.
Mmoja
wa wataalamu wa maswala ya kiteknolojia, anasema kuwa kampuni ya Apple
inapaswa kuchunguza malalamiko hayo na hata kutoa taarifa rasmi haraka
iwezekanavyo.
Jasdeep
Badyal anasema kuwa Apple inapaswa kujibu madai hayo na kisha ikiwa ni
kweli, basi inapaswa kuchukua hatua ya kuwapa simu mpya watu walioripoti
kuwa simu zao zimejipinda.
Aliongeza
kuwa hata kama kulikuwa na simu kdhaa tu zenye tatizo hilo, kampuni
hiyo inapaswa kutoa taarifa na kueleza kilichofanyika.
No comments:
Post a Comment