TTCL

EQUITY

Thursday, October 16, 2014

Migogoro ya ardhi Bunju Kionzile Inayodaiwa Kuendeshwa kinyume cha sheria Yadaiwa inachochewa na wenye Fedha.

Siku chache baada ya ITV kuripoti bomoabomoa ya kuacha zaidi ya wakazi 100 bila makazi katika migogoro ya ardhi eneo la bunju kionzile kata ya mabwepande iliyodaiwa kuendeshwa kinyume cha sheria mwenyuekiti wa baraza la aridhi kata hiyo Bw. Athmani Shomari ameibuka akieleza vitendo hivyo kuchochewa na wenye fedha kudharau mabaraza hayo hali ambayo inachochea ukuaji wa migogoro siku hadi siku.
Bw. Shomari ameyasema hayo mara baada ya mkutano wa wananchi waliobomolewa nyumba zao katika eneo la Bunju kionzile manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam waliokuwa wakiomba serikali kuingilia kati ili kuepusha maafa yanayoweza kujitokeza ambapo katika mazungumzo yake alieleza kupeleka shauri hilo ngazi ya wilaya kwa hatua zaidi kutokana na kumzidi uwezo baada ya nyumba kubomolewa.
 
Katika maombi ya wananchi kuiomba serikali pia wameliomba jeshi la polisi kutojihusisha na aina yoyote ya migogoro ya ardhi ili kuepuka matumizi ya nguvu yanayopelekea ukiukwaji wa haki za binadamu na kuyapa nafasi mabaraza ya ardhi yanayoanzia ngazi za kata huku kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni Bw. Kamilius Wambura kwa njia ya simu akieleza jeshi hilo kutojihusisha na masuala ya migogoro ya ardhi zaidi ya pale ambapo watahisi kuna uvunjifu wa amani kwa kulinda amani na si vinginevyo.
 
Uchunguzi wa ITV kupitia upimaji wa mradi wa viwanja elfu 20 vya jiji la Dar es salaam umebaini eneo linalogombewa kuachwa kama sehemu ya hifadhi ya mto wa mpiji ambao ni moja ya mito mikubwa ya msimu hapa jijini Dar es salaam ambao kisheria na unahitaji kuhifadhiwa kwa sheria za hifadhi ya mazingira na wakati huo huo inaelezwa kuwa eneo hilo limegawiwa kama makazi ya watu na wengine kuwa na hati miliki ikiwemo pia uwanja wa mazoezi ya timu ya simba.

No comments:

Post a Comment