WAKATI wadau wa afya wakihangaika kudhibiti vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua, imeelezwa kuwa wakina mama wengi wanakufa kutokana na harakati za utoaji mimba kwa njia zisizo salama.
Msimamizi wa miradi wa shirika la Path Finder,PATRCIK LEMA amebainisha hayo mjini Kigoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuibua hoja ya kuitaka serikali kuangalia upya sheria ya utoaji mimba ili kuwaokoa wanawake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama.
Lema amesema kuwa sheria inakataza wanawake kutoa mimba isipokuwa pale ambapo maisha ya mama yapo hatarini, lakini kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake wanaotoa mimba kwa njia ambazo si salama ambao wengi wao hufariki kutokana na matukio hayo.
Akizungumzia tatizo hilo Mwanasheria JULIUS TITUS amesema utoaji mimba usio salama ni changamoto kubwa katika kudhibiti vifo vya wanawake huku akizitaka asasi zisizo za kiserikali zianze kupaza sauti na kuamsha mjadala wa kitaifa kuhusu sheria ya utoaji mimba na mapungufu yake.
Awali Meneja Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Women Promotion Centre inayoendesha mradi huo, ABUBAKAR MTOKA alisema mradi huo unalenga kuona namna gani serikali inaangalia sheria ya utoaji mimba kunatokana na utafiti uliofanywa na shirika lake na kubaini kuwepo kwa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment