Mwenyekiti
wa baraza la wanaweke Chadema Halima Mdee amewataka wananchi wa Bukombe
mkoani Geita wasikubali kulazimishwa kuunga mkono katiba
inayopendekezwa waangalie kama katiba hiyo imezingatia maoni waliyo
yapendekeza yakiwemo ya kutaka rasilimali za nchi zilizopo zitumike
kunufaisha wananchi wote kwa usawa.
Mdee amesema wakati akizungumza na wanancchi wa Bukombe ambapo
amesema baadhi ya masuala yaliyowekwa kwenye rasimu inayopendekezwa
yakiwemo ya kilimo, uvuvi, ardhi na mifugo siyo kati ya mambo 14 ya
muungano na hayo ndiyo yanafanywa kuwa propaganda ya bunge maalumu la
katiba kuwa rasimu hiyo haijazingatia maoni ya watanzania huku ibara ya
22 kifungu cha pili kinamnyima haki mwananchi kudai haki zilizowekwa
ndani ya rasimu hiyo mahakamani.
Naye mjumbe wa mkutano mkuu wa Bawacha Upendo Peneza amesema
serikali imeshindwa kusimamia na kulinda rasilimali za watanzania kwa
baadhi ya wawekezaji wanaochimba madini katika migodi ya mkoa wa Geita
bila kulipa kodi kwa madai watahusika katika kufanya shughuli za
maendeleo zikiwemo kujenga shule na zahanati huku wachimbaji wadogo
wakiendelea kunyanyasika kwa kulipa kodi na kushindwa kujiendeleza
kiuchumi.
No comments:
Post a Comment