Kwa baadhi
ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine
ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona.
Mfungwa
mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za
mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini
mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
No comments:
Post a Comment