Southampton
imemsajili mchezaji wa Senegal Sadio Mane kutoka katika klabu ya
Austria ya Red Bull Salzburg kwa kima cha pauni milioni kumi.
Mchezaji
huyo mwenye umri wea miaka 22, ambaye ameingiza mabao, 45 katika mechi
87, wakati wa msimu wa ligi ya nchi hiyo, anaweza kucheza kama kiungo
cha kati , kwa mujibu wa meneja Ronald Koeman.
Southampton pia wamekamilisha hatua za kumsajili kwa mkopo mlinzi wa Ubelgiji Toby Alderweireld kutoka Atletico Madrid.
Alderweireld
alisaidia Atletico kushinda ligi ya uhispania ya La Liga ili kuweza
kufika fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshindia klabu yake mechi 37.
Koeman amenukuliwia akisema Alderweireld ni mlinzi mzuri na mchezaji mzuri sana.
Mchezaji
huyo wa Ubelgiji, ambaye alishinda mataji matatu katika misimu tisa
alipokuwa anachezea Ajax kabla ya kuhamia Madrid msimu uliopita, alisema
Koeman alimvutia kakama meneja.
No comments:
Post a Comment