Weekend hii pamoja na kusheherekea tamasha la pasaka katika mkoa wa 
Shinyanga, Edson Zako Mwasabwite anamshukuru Mungu kwani ni makubwa 
yangekuwa yamempata hadi hivi sasa. 
Muimbaji huyu nyota anayejulikana kwa wimbo wa "Ni kwa Neema tu" 
akitokea Dodoma kwenda Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 3 Mei, ndipo 
ajali ilitokea na maeneo ya Gairo, mwendesha bodaboda akiwa amembeba 
abiria walikatiza barabarani, ndipo hapo katika jitihada za kumkwepa 
akawa amemgonga, (abiria akaishia kwenye kioo cha gari, airbag 
zikafunguka hata asiweze kuona mbele hadi alipogota kwa kugonga gogo) 
ambapo mwenye bodaboda na abiria wake waliumia kiasi cha kupelekwa 
hospitalini (na kugundulika na polisi ya kwamba walikuwa wamelewa), 
ambapo wapo hadi hivi sasa, huku gari yake ikiwa kituo cha Polisi Gairo.
Edson akizungumza na GK, ameeleza kuwa anamshukuru Mungu maana ni mwema,
 hakika ni kwa Neema tu bado anaishi, ambapo alitoka salama, akiwa na 
maumivu ya shingo tu hadi hivi sasa, ambayo yanaendelea kutoweka
![]()  | 
| Edson Mwasabwite na Faraja Ntaboba kwenye tamasha la pasaka jijini Mwanza. | 



No comments:
Post a Comment