![]() |
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)kutoka Tanzania wakiteta,kutoka kushoto ni Shyrose Bhanji,Adam Kimbisa na Abdulah Mwinyi. |
![]() |
Mbunge Abdulah Mwinyi akizungumza jambo na wabunge wenzake,Twaha Taslima(kati)na Bernard Mulunya. |
![]() |
ARUSHA,Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limeanza kuonekana kufanana na Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Bunge
hilo jana limevunjika bila kujulikana litakutana tena lini baada ya
kuibuka mabishano ya kisheria kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Spika,
Margret Zziwa.
Hoja
ya kumng’oa Spika Zziwa ilianza kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari
vya Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa na hatimaye kuwasilishwa jana
na Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya kwa niaba ya wenzake Shy-Rose
Bhanji wa Tanzania, Nyiranilimo Odette wa Rwanda na Hafsa Mossi kutoka
Burundi.
Awali
Bunge hilo linalopaswa kuanza vikao vyake saa 8:00 mchana lilichelewa
kuanza hadi Saa 9:44 alasiri baada ya wabunge kugoma kuingia ukumbini
walipobaini kuwa hoja ya kumng’oa Spika haikuwa miongoni mwa shughuli za
Bunge kwenye kikao cha jana.
Baada
ya mashauriano ya muda mrefu kati ya ofisi ya spika, Mwanasheria wa
EAC, Wakili Wilbert Kaahwa na Katibu wa Bunge, Kenneth Madete, Spika
Zziwa alikubali hoja ya kumng’oa iongezwe kwenye orodha ya shughuli za
Bunge ndipo Mbunge Mathuki alipopewa fursa ya kuwasilisha hoja.
Hata
hivyo dakika moja tangu Mathuki alipoanza kusoma maelezo ya hoja hiyo,
Mbunge Fred Mukassa Mbidde aliinuka na kuomba mwongozo wa Spika na
alipopewa nafasi, alipinga hoja hiyo kuwasilishwa na kujadiliwa kwa
madai kuwa kuna kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ)
inayohusiana na hoja hiyo.
Akifafanua
Mbidde alisema kesi hiyo inaomba mwongozo na ufafanuzi wa kisheria
kuhusu kanuni ya 9 ya Bunge la EAC inayoelekeza utaratibu wa kumwondoa
madarakani Spika wa Eala iwapo kutatokea haja ya kufanya hivyo.
Wakati
Mbunge Mbidde akiwa bado amesimama huku akiendelea kutoa hoja yake,
Mbunge Joseph Ombasa kutoka Kenya aliinuka na kumpinga mbunge mwenzake
akisema anataka kulipotosha Bunge kwani kifungu 38 (3) kinaruhusu Bunge
hilo kujadili hoja yoyote yenye masilahi ya umma wa EAC ikiwamo hilo la
kumng’oa Spika.
Baada
ya hoja ya Ombassa, Mwanasheria wa EAC, Kaahwa alisimama kutoa
ufafanuzi wa kisheria licha ya kukiri kuwapo kesi mahakamani alisema
tayari mahakama hiyo imetoa uamuzi mdogo kuwa shauri hilo haliwezi
kuzuia shughuli na mjadala wowote wenye nia ya kumwondoa Spika
madarakani
Hoja
hiyo ya Mwanasheria ilimwibua tena Mbunge Mbidde aliyehoji kwanini
maelezo na ufafanuzi wa mwanasheria huyo yanatoa mwelekeo wa ulipo
msimamo wake kuhusu hoja iliyokuwa mbele ya Bunge.
Katika
hali iliyoashiria uwapo wa kimkakati kati ya kiti cha Spika na Mbunge
Mbidde, Spika Zziwa naye aliunga mkono hoja ya mwanasheria kuonekana
anaelemea upande unaotaka ang’olewe.
Kauli
hiyo ilimwamsha kitini Mwanasheria Kaahwa aliyemhakikishia Spika kuwa
hoja yake inalenga kusaidia uendeshaji bora wa Bunge na siyo kuegemea
upande unaotaka kumng’oa.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment