Thursday, April 3, 2014
ANGALIA PICHA ZA MWALIMU KAHABA ETI MSHAHARA HAUTOSHI
Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
Wakati Wakristo bado wapo kwenye Kwaresma, mama aliyejitambulisha kuwa
ni mwalimu wa shule ya msingi, amenaswa laivu akijiuza maeneo ya
Mbagala-Zakhem jijini Dar.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 24,
mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa
Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani
ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina wakiwemo mabinti
wadogo.Chanzo hicho kilimwaga data kuwa, kuna mzee maarufu kwa jina la
babu katika eneo hilo ambaye amekuwa akiwapa machangudoa hifadhi katika
banda lake na kuwapa magodoro chakavu kwa malipo ya shilingi elfu moja
kwa kila kichwa.
KISIKIE CHANZO
“Jamani kwenye danguro hili kila aina ya uchafu upo. Wanatukwaza sisi
Wakristo ambao tupo katika kipindi hiki cha Kwaresma,” kilitiririka
chanzo hicho cha kuaminika maeneo hayo.
OFM KAZINI
Ili kujiridhisha na taarifa hizo, makamanda wawili wa OFM walitimba
katika danguro hilo wakajifanya wateja ambapo walimchukua mmoja na
kubaini kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi.
Mwalimu
na wenzakw wakiwa chini ya ulinzi.
TUJIUNGE NA CHANGU MWALIMU
“Kaka ongea fasta nipe changu, usinione hivi mimi ni mwalimu wa msingi,
mshahara haukidhi halafu isitoshe serikali haijatulipa malimbikizo yetu,
watulipe bwana pengine tunaweza kujikwamua,” alisema changu huyo ambaye
alimtaka kamanda wa OFM alipie shilingi elfu kumi kama malipo ya huduma
tendo moja.
POLISI WAITWA
Baada ya kujiridhisha kwa uwepo wa biashara hiyo, OFM waliwapigia simu
polisi wa Kituo cha Kizuiani, wakafika na kufanikisha zoezi la
kuwakamata machangu wapatao 16 pamoja na babu anayewapa hifadhi ili
wauze miili.
..Wakiingizwa
kwenye gari la polisi.
VIBANDA KIBAO VYABAINIKA
Wakati zoezi la kuwakamata likiendelea maeneo hayo, vilibainika vibanda
vingi ambavyo machangu hao hufanyia uchafu wao pamoja na mfuko mkubwa
ambao madadapoa hao huhifadhia nguo zao za heshima kabla hawajaingia
‘mzigoni’.
WAACHA WATOTO NYUMBANI
Baadhi ya machangudoa hao waliotiwa mikononi mwa polisi, walikiri kuwa
wamewaacha watoto wao nyumbani huku wengine wakidai ni wake za watu
hivyo kuomba wasipigwe picha kukwepa aibu pindi zitakapochapishwa
gazetini.
Watuhumiwa wakiwa kwenye gari la polisi chini ya ulinzi mkali.
“Jamani msitupige picha sisi wengine tuna watoto na waume zetu, tunaomba
msamaha jamani,” walisikika madadapoa hao.
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya kamatakamata kukamilika, machangu hao pamoja na mzee huyo
walipandishwa kwenye difenda la polisi na kupelekwa katika Kituo cha
Polisi Kizuiani kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa
Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka ya uzururaji.
SOURCE:GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment