Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema
alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye
alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu
kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa
Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda
ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu
tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti
gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya
machizi wote, ohooo!”
MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na
kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka
tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia
wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara
cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi,
Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini
kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale
alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo
lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi
ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na
wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake
walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa
kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa
picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika
mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile
viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo
mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!
Wema
akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na
wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake
walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa
kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa
picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika
mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile
viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo
mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!
Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na
majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha
Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake
wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua
zao.
Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo
mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga
mtaa.
Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku
wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku
peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!
APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika
lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili
kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu
walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.
Gari lake lililomleta Global kufanya timbwili.
KWA NINI?
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye
na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na
mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria
vitendo vya usagaji.
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
No comments:
Post a Comment