ELIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.

Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara
kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo
jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua
wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.
Lulu |
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna
kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana
ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata
katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”
Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”

No comments:
Post a Comment