Geez
Mabovu mtoto wa Doll South yuko katika hali mbaya kiafya na amelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuzidiwa ghafla wakati
akisubiri kufanya show mjini humo akiwa na Jan B na Songa. Songa
ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwaopa taarifa fans wa Mabovu
na kuwaomba waendelee kumuombea. “ASANTENI SANA IRINGA,SIKUTEGEMEA MNAPENDA HIP HOP KIASI KILE...MLITISHA
SANA. ILA KUNA HABARI MBAYA NDUGU YETU GEEZ MABOVU HALI YAKE SIO NZURI
AMELAZWA,NAOMBA TUMUOMBEE ARUDI KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA. ASANTENI”
Songa ameueleza mtandao wa Bongo5 kuwa Mabovu alizidiwa ghafla kabla ya show na akapelekwa hospitali ya mkoa. Mapema jana ,Geez Mabovu aliongea na tovuti ya Times Fm na kueleza kuwa alienda nyumbani kwao Iringa ambapo alikuwa hajaenda kwa muda mrefu na kwamba alienda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa (December 25) na familia yake. Rapper huyo aliongeza kuwa ameamua kuacha kutumia pombe kuanzia January Mosi mwakani kutokana na kutaka kufanya mabadiliko zaidi katika maisha yake. Tumuombee Geez Mabovu apate nafuu na apone haraka.
No comments:
Post a Comment