Hapa ni sehem maalumu itakayowekwa ball drop 2013 kuashiria mwaka
mpya. Times Square New York City ni sehem maarufu sana kwa sherehe za
kushuhudia ball drop hilo kila mwaka. Watu kutoka sehemu mbali mbali za
Marekani na dunia hufika hapa kila mwaka na kushuhudia ball hilo kwa
mbwebwe nyingi kama kukiss na hata watu wengine kupropose kwa wachumba
zao ili kuanzisha safari ndefu ya kimapenzi hadi ndoa.
Hii ndiyo taswira ya sehemu hii maalum kwa live performance wakati
watu wakisubiri kuona ball likidondoka. Hata kukiwa na snow au mvua watu
huingia sehemu hii mapema kabisa kuanzia saa 4 asubuhi na watakaa hapo
hadi saa 6 usiku bila hata kujigusa. Watu wengine hudiriki kwenda na
chakula na hata mifuko wa kujisaidia haja ndogo. Hufanya hivyo ili
kujihakikishia nafasi ya kuona live performance na ball drop la
kuashiria mwaka mpya kwa karibu kabisa.
Traffic za magari zimepungua baada ya police kufunga baadhi ya
barabara kwa ajili ya mkesha huo wa mwaka mpya katika maeneo ya times
square NY.
Unaweza kuona uzio wa kuzuia watu kuingia katikati ya barabara mapema kabla ya wakati.
Jamaa huwezi kuamini licha ya kuwa na baridi ya 27 degress lakini
kifua nje na boxer yake akitoa burudani katika eneo ilo la times square
NY. Ukitaka kupiga picha na jamaa huyu unatakiwa kutoa tips ya dola 2
kwani kazi na dawa.
Afisa wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani kutoka Washington DC bwana Misana akipata ukodak na mwenyeji wake Ny Ebra katika maeneo ya Times Square NY. |
Bwana Misana akiwa na familia yake maeneo ya Times Square NY. |
Unaweza kuona watu ni wengi kiasi gani licha ya kuwa na hali ya hewa ya baridi katika jiji New York kwa sasa. |
No comments:
Post a Comment