Askari wa Kikosi cha Zima moto na
Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar
Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Hassan ambaye alipanda juu ya mnara huo
kwa lengo la kufikisha ujumbe wa kutaka kuonana na Rais Kikwete ili
aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia
kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na
Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya
kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo
Jijini Dar Es Salaam Leo
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji
Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na
Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya
kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata
madhara
Kijana aliyefahamika kwa jina moja la
Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya
Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi
uliopita Ubungo jijini Dar
Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia.
Raia wakishuhudia tukio hilo
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar leo
Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa limetia timu eneo la tukio kwaajili ya Kuokoa
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia gari
la Polisi likiondoka na Kijana Hassan ambaye alipanda juu ya Mnara leo
Ubungo jijini Dar Es Salaam
No comments:
Post a Comment