Mwanamuziki
nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja
joto
ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa
kila kitu
pamoja na gari yake.
Mwanamuziki
huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta
Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafla kundi la watu watano
lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na
kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao
wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu.
Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.
No comments:
Post a Comment