TTCL

EQUITY

Tuesday, November 12, 2013

NI HUZUNI; DK. SENGENDO MVUNGI UMETUTOKA....

TAARIFA ZA KUSIKITISHA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE NI KWAMBA DOKTA MVUNGI ALIYEKUWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU AMEFARIKI DUNIA

Marehemu Dk. Mvungi Enzi za uhai wake


Marehemu akiwa mahututi akipelekwa Afrika ya kusini

Kutoka Hospitali ya Milpark jijini Johannesburg Afrika Kusini; Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dr. Sengondo Mvungi amefariki dunia hospitalini hapo leo majira ya saa tisa alasiri alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. 
 
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Hospitali alimokuwa amelazwa Marehemu Dk. Mvungi baada ya kuamishwa kutoka Muhimbili Jijini Dar es salaam nchini  Tanzania

 Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wanaharakati wote kwa kuondokewa na Dk Sengondo Mvungi ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi, Bwana alitwaa Bwana ametoa Jina lake libarikiwe.

No comments:

Post a Comment