Kwa
dada zangu wote wa kizazi hiki chetu: Sababu zinazoweza kukufanya ukose
mchumba ukabaki singo muda mrefu au maisha yote huku unalialia:
1. Kutokuwa na hofu ya Mungu. Binti huenda kanisani wala msikitini upo
tu nyumbani. Mvulana serious akikuangalia ataona ni mtu wa kutumika tu
na si mtu unayeweza kulea watoto katika misingi ya maana na kuwa
muhimili wa familia.
2. Masaa 24 wewe uko kwenye simu na TV.
Ukitoka channel hii unahamia ile. Tamthilia zote unazijua wewe. Hebu
niambie kichwa chako kitakuwa kimejaa nini zaidi ya mapenzi ya
Kifilipino na Kimeksiko ya kwenye hizo tamthlia?
3. Hutaki kufanya majukumu ya msingi ya kike kama kupika na kuosha
vyombo, kisa TV na sinema zimekuonyesha kuwa hayo pia ni majukumu ya
wanaume. Hii ni Afrika mama, utaumia. Unaenda kwa mpenzi wako
kumtembelea vyombo unakuta vichafu huoshi, unakaa tu. Unajishushia
pointsi. Osha na mwambie si vizuri kuacha vyombo vichafu.!
4.
Kuwa mtumwa wa kila kitu kipya. Mtu gani atapenda kuwa na mwanamke
ambaye ni mtumwa wa kila aina mpya ya simu, kila aina mpya ya kiatu,
kila aina mpya ya nguo, kila saluni mpya anataka kwenda?
5. Kutumia vipodozi hadi unapitiliza. Badala ya kuvutia unatisha!
6. Muda mwingi kutumia kwenye mitandao. Mara Twitter, Mara Facebook,
mara Instagram! Wataalam wanasema binadamu ana uwezo wa kuwa na marafiki
si chini ya 150 tu. Lakini wewe kila mtandao una watu 2,000! Sasa hivi
unaweza kuona haina maana ila ngoja ufike miaka 35 ukiwa single and
searching ndo utaelewa.
7. Acha kutoa namba yako kwa kila
mwanaume! Hakuna mwanaume ambaye anataka kuwa na mwanamke ambaye kila
muda anawasiliana na watu hata wasioeleweka.
8. Jipe thamani na
ongeza thamani kwenye maisha ya mpenzi wako. Kama uko shule soma, kama
unafanya kazi fanya vizuri, kama una biashara jitume na kila mara
mshauri vizuri mpenzi wako. Hakuna mwanaume anataka kukaa na mwanamke
ambaye yupo yupo tu!
9. Acha tabia ya kila saa kuruhusu marafiki zako kuongoza maisha yako. Kuwa na misimamo yako.
10. Kutembea tembea na makundi ya wasichana wenzako kila mahali. Kwani
lazima? Huwezi kutembea mwenyewe? Inawezekana kabisa katika kundi la
wasichana wenzako yuko ambaye ana tabia za ajabu na mwanaume akimuona tu
na wewe atakuhukumu kwa kuwa mko kundi moja. Sio muda wote ni muda wa
kutembea na kundi la marafiki.
Naachia hapa kwa leo.
No comments:
Post a Comment