TTCL

EQUITY

Saturday, November 2, 2013

LULU AWAKERA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WA BABA YAKE WEMA MARA BAADA YA KUTOA CHEKO LA 'KISHANGINGI' WAKATI IBADA IKIENDELEA..!!

KATIKA hali isiyotarajiwa, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenaswa na kamera yetu akiangua kicheko cha nguvu huku misa ya msiba ikiendelea.
Tukio hilo lililowaacha midomo wazi waombolezaji lilitokea Jumanne iliyopita nyumbani kwa marehemu baba wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, Isaac Abraham maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar wakati Lulu alipokuwa amekwenda kumfariji mwigizaji mwenzake huyo.

Lulu (wa pili kushoto) akiangua kicheko na shosti wake wakati misa ya msiba ikiendelea. 

Lulu ambaye alikuwa amevalia sare maalumu waliyovaa watu wa karibu na familia ya marehemu, alinaswa akiwa amejisahau kabisa kama yupo msibani na kuanza kupiga stori na dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
...Wakizidi kupiga stori na kufurahi wakati  ibada ikiendelea.
Mh! Sasa mwenzetu pale amepitiliza haiwezekani ajisahau kiasi kile wakati hapa ni msibani. Atachekaje kiasi kile, hii ni aibu jamani bora hata wangeenda kuchekea pembeni,” alisikika mmoja wa waombolezaji.
Baada ya kugundua papararazi wetu anawafotoa picha, ghafla wawili hao walihamaki na kuacha kucheka huku wakijiziba usoni wasiweze kunaswa sura zao kiurahisi na kamera.
Katikati ya wiki hii, Lulu aliripotiwa kuwa amevurumusha matusi kwa mapaparazi katika msiba huohuo hali ambayo inawafanya mashabiki wahoji kulikoni?

No comments:

Post a Comment